Nani aanze, nani asubiri vs Namungo Fc leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Nov 2020
Nani aanze, nani asubiri vs Namungo Fc leo?

Ifikapo saa moja usiku wa leo, Yanga itakuwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa kumenyana na Namungo Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Huu ni mchezo muhimu sana kwa mabingwa hao wa kihistoria kwani wanahitaji kuondoka na alama zote tatu ili kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi

Ni wazi kocha Cedric Kaze ataingia kwenye mchezo huo akiwa na kikosi chake kamili

Yawezekana kile kikosi kilichoanza mchezo dhidi ya Simba, kikashuhudiwa tena leo pale kwa Mkapa

Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustafa, Lamine Moro na Bakari Nondo Mwamnyeto, ndio wanaounda ukuta wa chuma wa Yanga

Feisal Salum 'Fei Toto' na Mukoko Tomombe wameunda pacha 'konki' pale eneo la kiungo wakati Farid Mussa na Tuisila Kisinda wao wameaminiwa sana wakishambulia kutokea pembeni

Pengine mabadiliko yanayoweza kutarajiwa ni kuingia kikosini kwa Carlinhos ambaye tangu aliporejea kutoka kwenye majeraha, kiwango chake kimemvutia Kaze

Safu ya ushambuliaji ya Yanga imekuwa ikiwategemea zaidi Michael Sarpong, Ditram Nchimbi, Yacouba Sogne na Waziri Junior, mfumo atakaotumia Kaze ndio utaamua nani aanze kati yao

Huu ni mchezo wa tatu Yanga inacheza na Namungo Fc kwenye ligi. Michezo miwili iliyopita timu hizo zilitoka sare. Yanga itakuwa ikisaka ushindi wake wa kwanza dhidi ya Namungo Fc katika mechi za ligi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’