Wakati akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alihoji kitendo cha TFF kukalia kimya kesi mbili walizozipeleka kuhusu nyota Bernard Morrison na ile ya kipa Ramadhani Kabwili.
Kesi ya Kabwili ni ya muda mrefu zaidi lakini inashangaza mpaka sasa hakuna taarifa iliyotolewa na TFF kuhusu mwenendo wake
Cha kushangaza Simba ilipeleka madai ya kuhujumiwa hivi karibuni na tumeona baadhi ya viongozi wakihojiwa na Jeshi la Polisi
Mwakalebela amesema kesi ya Kabwili waliipeleka ushahidi TAKUKURU na majibu walipewa TFF lakini wamekaa kimya pengine kwa kuwa suala hilo linaihusu klabu ya Simba
Aidha kuhusu kesi ya mkataba wa Morrison, Mwakalebela ameitaka TFF itoe majibu wakati huu ambao bado dirisha dogo la usajili halijafunguliwa kwani litakapofunguliwa Simba watakuwa na nafasi ya kurekebisha mapungufu yaliyopo kwenye mkataba huo ambao Morrison alisaini baada ya kutangazwa kuwa mkataba wake na Yanga ulikuwa batili