Mechi mbili za kuipeleka Yanga kileleni VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Nov 2020
Mechi mbili za kuipeleka Yanga kileleni VPL

Keshokutwa Jumapili, kikosi cha Yanga kitashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Namungo Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom

Siku tatu baadae, Yanga itaelekea kule Chamazi Uwanja wa Azam Complex kuwakabili vinara wa ligi Azam Fc

Mechi hizi mbili zinaweza kuipeleka Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi kama itafanikiwa kushinda zote

Azam Fc wanaongoza ligi wakiwa na alama 25 wakati Yanga wakiwa nyuma yao wakijikusanyia alama 24. Wakati Yanga ikicheza na Namungo Fc, mchezo unaofuata kwa upande wa Azam Fc ni dhidi ya KMC

Aidha, kuelekea mchezo wa Jumapili, Cedric Kaze, Mkufunzi wa Yanga amesema vijana wake wako tayari kupigania alama tatu muhimu ili waendelee kubaki katika nafasi nzuri kwenye mbio za ubingwa msimu huu

Kaze amethibitisha kuwa nyota wake nahodha Lamine Moro na Carlinhos wako fit kuelekea mchezo huo

Lamine alirejea kikosini juzi baada ya kupona majeraha aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Simba

Carlinhos alikuwa nje kwa takribani wiki tatu, kabla ya kurejea kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’