Mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Namungo Fc utapigwa Jumapili Novemba 22 uwanja wa Benjamin Mkapa
Kulingana na ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi baada ya kufanyiwa mabadiliko katika baadhi ya mechi za raundi ya 12, mchezo huo utapigwa kuanzia saa moja usiku
Uwanja wa Mkapa ulifungwa mwezi uliopita ukifanyiwa maboresho kwa ajili ya kutumika mchezo wa Afcon dhidi ya Tunisia ambao ulipigwa jana na kumalizika kwa matoeo ya sare ya bao 1-1
Mchezo dhidi ya Namungo utakuwa wa kwanza kwa kocha Cedric Kaze kucheza katika uwanja wa Mkapa
Aidha, mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Novemba 25, utakuwa mbashara dimba la Azam Complex

ADVERTISE HERE