Mfungaji bao la mwisho kuzawadiwa gari

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Nov 2020
Mfungaji bao la mwisho kuzawadiwa gari

Achana na ahadi ambazo GSM wamewaahidi wachezaji iwapo wataibuka na ushindi dhidi ya Simba leo, umoja wa mashabiki wa Yanga nao wameweka mezani zawadi kemkem kwa ajili ya wachezaji

Akizungumza na wanahabari jana, Msemaji wa Mashabiki wa Yanga Jimmy Msindo 'Kindoki' alisema kuwa wao kama mashabiki watatoa kitita cha Tsh Milioni moja kwa kila bao litakalofungwa kwenye mchezo huo

"Hapa mkononi tunazo fedha nyingi tu kwa ajili ya wachezaji wetu. Tunachotaka ni wao kutupa furaha tu siku ya kesho (leo). Tutanunua kila goli watakalofunga kwa Tsh Milioni moja. Wakifunga bao moja watapata Milioni moja, wakifunga bao tano watapata Milioni tano na fedha zitaongezeka hivyo hivyo kulingana na idadi ya magoli," alisema Msindo

"Lakini pia tunayo zawadi kubwa zaidi, mchezaji atakayefunga bao la mwisho tutamzawadia gari aina ya Toyota Subaru Impreza. Tunataka kila mchezaji atakayecheza awanie fursa hii ya kufunga bao la mwisho ili tumzawadie gari hili," aliongeza Kindoki

Hamasa ya mashabiki wa Yanga imekuwa kubwa kuelekea mchezo huu. Uimara wa kikosi chao unawapa mashabiki kila sababu ya kujiamini kuwa wataondoka na alama zote tatu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’