Kaze anazitaka alama zote tatu za Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Nov 2020
Kaze anazitaka alama zote tatu za Simba

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Cedric Kaze amesema mkakati wake mkubwa ni kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Simba SC unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa Jumamosi katika uwanja wa Benjamin  Mkapa jijini Dar es salaam

Yanga ilirejea Dar es salaam juzi usiku wakitokea mkoani Mwanza ambako walilazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Gwambina Fc

Katika mchezo huo kaze alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi alichotumia, akiupigia hesabu mchezo dhidi ya Simba

Akizungumza baada ya mchezo juzi, Kaze alisema mchezo dhidi ya Simba ni mkubwa na wanahitaji kuwa na maandalizi mazuri

"Ni mechi kubwa sana na Watanzania wote watakuwa wanaiangalia, nina imani itakuwa mechi nzuri sana. Mimi na vijana wangu tutajipanga kushinda mechi hii," alisema Kaze

Mchezo unaozikutanisha Yanga na Simba mara nyingi huwa na presha kubwa kwa kuwa ndio mchezo unaotizamwa zaidi na mashabiki wa soka Tanzania na hata ukanda wa Afrika Mashariki

Kaze amesema wamepata nafasi ya kuwafuatilia wapinzani wao hivyo wanafahamu ni mbinu gani wataitumia ili kuweza kuondoka na alama zote tatu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’