Nkomolla akaribishwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Dec 2017
Nkomolla akaribishwa Yanga
Yanga tayari imekamilisha usajili wa wachezaji wawili katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Wakwanza alikuwa mlinzi mahiri wa kati Fiston Kayembe Kanku kutoka DRC ambaye amejaza nafasi moja ya Kimataifa iliyokuwa imebaki.

Wapili ni mshambuliaji kinda Yohana Nkomolla aliyesajiliwa kutoka kikosi cha timu ya taifa ya vijana Ngorongoro Heroes iliyoshiriki michuano ya AFCON U17 mapema mwaka huu nchini Gabon.

Nkomolla ametambulishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika na kumkaribisha rasmi katika familia ya Yanga.

Nyika amelitaka benchi la ufundi kuhakikisha linalinda kipaji cha mshambuliaji huyo kinda kwani ni hazina kubwa ya Yanga baadae.

"Tunahitaji kuwa na vijana ambao watakuwa wakiwa ndani ya klabu,hii itawafanya kujua misingi na utamaduni wetu Kabla kuwa wachezaji wakubwa baadae, ana kipaji kikubwa,ni jukumu la benchi la ufundi kukiendeleza kwa manufaa ya klabu siku za usoni," alisema Nyika.

Uongozi wa Yanga umedhamiria kukisuka upya kikosi chake ambapo sasa kimesheheni idadi kubwa ya wachezaji vijana ambao watakuwa tegemeo siku za usoni.

Baadhi ya wachezaji vijana walio chini ya umri wa miaka 23 ndani ya kikosi cha Yanga sasa ni pamoja na Benno Kakolanya, Ramadhani Kabwili, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Abdallah Shaibu, Maka Edward, Geofrey Mwashiuya, Emanuel Martin, Said Mussa, Baruani Yahya, Juma mahadhi, Matheo Antony, Said Juma, Pato Ngonyani, Pius Buswita, Raphael Daudi, Obrey Chirwa, Yohana Nkomolla, Ibrahim Ajib na Yusuph Mhilu
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’