Tambo zaanza mapemaa, mpambano wa watani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Nov 2020
Tambo zaanza mapemaa, mpambano wa watani

Mashabiki wa Yanga wametamba kuwa ni vyema watani zao Simba wakamkatia tiketi Kocha Mkuu wao, Sven Vandenbroeck kwani wana uhakika baada ya dakika 90 za mchezo baina yao Jumamosi hii, Mbelgiji huyo atatupiwa virago vyake.

Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana siku hiyo katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Tayari homa la pambano hilo imeanza kupanda kwa timu zote hizo, kila moja ikipanga mikakati ya kuibuka na ushindi ili kuwapa raha mashabiki wao.

Ukiachana na suala zima la pointi tatu, ushindi baina ya timu hizo kongwe hapa nchini, una maana kubwa kutokana na utani wa jadi uliopo kati yao

Hata hivyo, Yanga ndio wanaoonekana kupania zaidi kushinda ili kulipa kisasi cha kufungwa mabao 4-1 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports, hatua ya nusu fainali msimu uliopita.

Kwa upande wa Ligi Kuu Bara, Yanga ndio wenye rekodi ya kujivunia kwani msimu uliopita, walivuna pointi nne kati ya sita kutoka kwa watani wao hao baada ya kupata sare ya mabao 2-2 mzunguko wa kwanza, kabla ya kushinda bao 1-0 waliporudiana.

Utamu zaidi katika mchezo wa Jumamosi, ni kutokana na hali ya timu hizo katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga wakiwa wamewaacha Simba kwa pointi sita.

zote zikiwa zimecheza mechi nane, Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 22, wakati Simba wanakamata nafasi ya tatu na pointi zao 16.

Kutokana na hali hiyo, Simba watakuwa wakipania zaidi kuifunga Yanga Jumamosi ili kupunguza pengo la pointi kama moja ya mkakati wao wa kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu wa nne mfululizo.

Kwa kufahamu hilo, Yanga wameibuka na kutamba kuwa watani wao hao wa jadi, wasitarajie ushindi Jumamosi zaidi ya kipigo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’