Chimbuko la klabu ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Oct 2020
Chimbuko la klabu ya Yanga

Historia adhimu ya Yanga, maneno ya Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM

1910 - Navigation FC
1926 - 1928- Italiano FC
1930 - New Youngs FC
1935 - YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
1948 - hapo ndipo tulipata rangi zetu rasmi za ( KIJANI, NJANO & NYEUSI)
- alama ya mwenge.
- Ramani ya afrika katika NEMBO YA KLABU YETU.

Aidha, kabla ya uhuru chama cha TANGANYIKA AFRICAN ASSOCIATION ( TAA ) kilichoanzishwa mnamo 1929 kwa muda mrefu kilikuwa kikisumbuliwa na WAKOLONI, hapo ndipo TAA iliitumia klabu YANGA kwa ajili ya harakati za kupigania uhuru wa nchi yetu. Vikao vya siri na mpango mkakati ulikuwa ukifanywa na waasisi wa nchi hii kupitia mwamvuli wa YANGA.

Mahusiano hayo yaliendelea baada ya kuzaliwa TANU 1954 mpaka kufanikiwa kupata UHURU WETU mnamo tarehe 9 Disemba 1961 chini ya BABA WA TAIFA - HAYATI Mwl. JULIUS KAMBARAGE NYERERE.

Leo hii wadhamini, Viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wa timu iliyoshiriki kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye mikono ya wakoloni ilifanya ziara ya kutembelea nyumbani kwa BABA WA TAIFA na kufanikio kuzuru kaburi lake lililopo kijijini MWITINGO wilaya ya BUTIAMA mkoani MARA.

Mapokezi makubwa ya kihistoria yalifanywa kwa ukarimu mkubwa wa MAMA WA TAIFA LETU - Bibi MARIA NYERERE, mpenzi na mwananchama wa klabu ya YANGA!

Ama hakika mchango wa klabu yetu ya YANGA ya kusaidia kupigania UHURU utabaki katika kumbukumbu za vitabu vya kihistoria vya taifa hili la TANZANIA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’