Yanga kusaka rekodi mpya Musoma Jumamosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Oct 2020
Yanga kusaka rekodi mpya Musoma Jumamosi

Keshokutwa Jumamosi, mabingwa wa kihistoria Yanga watakuwa Mara kuwakabili wenyeji wao Biashara United katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom raundi ya nane

Huu ni mchezo ambao kama Yanga watashinda, watapanda juu ya msimamo wa ligi kwani watawapiku Azam Fc wenye alama 21 wakiwa wamecheza mchezo mmoja zaidi ya Yanga

Azam Fc ilipoteza mchezo wa kwanza msimu huu kwa kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar katika raundi iliyopita

Hata hivyo mchezo dhidi ya Biashara United hautarajiwi kuwa mwepesi kutokana na ubora wa timu zote

Biashara United wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia alama 16 baada ya kushuka dimbani mara nane

Wamekuwa na mwenendo mzuri wanapocheza katika uwanja wao wa nyumbani, kati ya mechi tano walizoshinda, nne wamepata ushindi nyumbani

Lakini pia Yanga haijawahi kupata ushindi dhidi ya Biashara United katika mechi zilizocheza uwanja wa Karume Musoma

Tangu Biashara walipopanda daraja, wamekutana na Yanga uwanja wa Karume mara mbili, wameshinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mwingine

Hivyo mchezo wa Jumamosi, Kocha Cedric Kaze atakuwa na jukumu la kuhakikisha anaandikisha historia mpya kwa kuipa Yanga ushindi wake wa kwanza hapo Musoma

Vijana wa Yanga wako 'onfire' baada ya kushinda mechi sita mfululizo ligi kuu, huu ni mchezo mwingine ambao hesabu zote zimeelekezwa katika 'kusepa' na alama zote tatu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
5h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
10h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’