Umwamba hauhitajiki kuhamasisha watu kuiunga mkono Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Oct 2020
Umwamba hauhitajiki kuhamasisha watu kuiunga mkono Stars

Jana ilisambaa 'clip' ya video ikimuonyesha Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Manara ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Hamasa Stars akiwatahadharisha mashabiki watakaoishangilia Tunisia itakapokuja kucheza na Tanzania mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za Afcon 2021

Manara alisema watu hao hawatakuwa Wazalendo na watastahili kuchukuliwa hatua na Mamlaka za Serikali itakapotokea wameingia uwanjani kuishangilia Tunisia

Kwa siku za karibuni baadhi ya mashabiki wa Yanga wamepaza sauti zao kutangaza kutoiunga mkono TFF na kuwa tayari kuishangilia Tunisia itakapokuja nchini kutokana na kile wanachokiita dhurma zinazofanywa na TFF kwa timu yao

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kuhusu hali ya upendeleo ambao Wanayanga wanadhani TFF wanaifanyia klabu ya Simba waziwazi

Yapo matukio mengi tu ambayo yanaweza kuthibitisha tuhuma za Wanayanga kwa TFF

Sakata la karibuni la winga Bernard Morrison ni mfano hai. Pamoja na Yanga kufungua madai lukuki kuhusu uhalali wa mkataba wa mchezaji huyo na Simba, hakuna chochote kilichofanyika

Ikumbukwe hadi wakati huu, kwenye mfumo wa usajili wa FIFA Morrison anatambulika kuwa mchezaji wa Yanga

Lakini pia Yanga imefungua malalamiko mengi TFF huko nyuma lakini huwa hayafanyiwi kazi. Ni juzi tu TFF imekanusha tuhuma hizo ambazo ziliibua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii

Manara alikwenda mbali zaidi kwa kutumia hoja ya kuwa wakati TFF ilipokuwa chini ya Rais Jamal Malinzi Simba nao walikuwa na malalamiko mengi lakini hawakuwahi kususia kuiunga mkono timu ya Taifa

Hoja hii ni sawa na kuhalalisha kile kinachofanywa na TFF dhidi ya Yanga eti kwa kuwa hata Malinzi aliwafanyia Simba. Hivyo Wanayanga hawapaswi kulalamika hata ikitokea wameonewa waziwazi!

Nadhani njia sahihi ya kumaliza sintofahamu iliyopo ni wadau kukutanishwa kuzungumza changamoto zilizopo na kutafuta suluhisho

Wanayanga ni Wazalendo kwani miaka yote wameiunga mkono timu ya Taifa, yanayotokea sasa ni katika kujaribu kutafuta njia TFF waweze kusikiliza malalamiko yao kwani yaonekana njia zote za kawaida zimekwama

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’