Ukuta matata, dakika 450, wameruhusu bao moja

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Oct 2020
Ukuta matata, dakika 450, wameruhusu bao moja

Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Fegurson aliwahi kusema kuwa safu bora ya ushambuliaji itakupa ushindi katika mechi lakini safu bora ya ulinzi itakupa ubingwa

Kauli hii inadhihirisha umuhimu wa kuwa na safu bora ya ulinzi linapokuja suala la kushinda ubingwa

Msimu huu safu ya ushambuliaji ya Yanga imeanza kwa mwendo wa kinyonga, pengine ni kutokana na ugeni wa wachezaji katika eneo hilo

Hata hivyo safu ya ulinzi imeiweka timu salama, ikiwa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 13 sawa na mabingwa watetezi Simba ambao wanatamba kuwa na safu bora ya ushambuliaji

Msimu uliopita, eneo la ulinzi lilikuwa tatizo kubwa kwa Yanga, ilikuwa sio rahisi sana kwa Yanga kuondoka na 'cleansheet'

Msimu huu mpaka sasa Yanga ina cleansheet nne kwenye ligi, ukuta wa Yanga uliruhusu bao pekee katika mchezo wake wa kwanza msimu huu dhidi ya Tanzania Prisons

Tangu wakati huo hakuna bao walilofungwa tena iwe kwenye ligi na hata michezo ya kirafiki

Ni kazi kubwa inayofanywa na manahodha Lamine Moro na Bakari Nondo Mwamnyeto ambao ndio wanasimama mbele ya mlinda lango Metacha Mnata

Hawa wanasaidiana na walinzi wa pembeni Kibwana Shomari, Yassin Mustafa, Deus Kaseke na Adeyum Saleh kwa nyakati tofauti bila ya kuwasahau viungo zawadi Mauya, Tonombe Mukoko na Feisal Salum ambao kwa wastani wameshirikiana  katika mechi kadhaa

Kocha Cedric Kaze ana kazi moja tu, kuhakikisha anatengeneza muunganiko pale mbele ili kuzalisha mabao mengi

Huku kwenye ulinzi hapaswi kuwa na wasiwasi kwani tayari anao watu wa kumuhakikishia ubingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’