Cedric Kaze mkufunzi mpya wa Yanga, jana alianza rasmi majukumu yake ya kuwanoa mabingwa hao wa kihistoria
Mazoezi yake ya kwanza yamedhihirisha ni aina gani ya timu anakwenda kutengeneza
Jambo la kufurahisha zaidi ni mwitikio wa wachezaji, kila mmoja ana shauku ya kuingia katika kikosi cha Mrundi huyo
Baada ya kutua Kigamboni juzi, Kaze alipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji akibainisha mipango yake huku akiwahakikishia kuwa wote wana nafasi sawa kwenye kikosi chake muhimu wanapaswa kuonyesha kile walichonacho



Mwamba huyu amekuja na jambo lake, hakuna shaka Wanayanga hawatajutia uwepo wake katika timu yao
ADVERTISE HERE