Kamati itaweza kumaliza 'mgomo' wa mashabiki Stars?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Oct 2020
Kamati itaweza kumaliza 'mgomo' wa mashabiki Stars?

Ukweli ni kuwa Wanayanga walio wengi wamepoteza imani na uongozi wa Rais wa TFF Wallace Karia kutokana na kile kinachoonekana klabu yao kutotendewa haki katika masuala mengi ndani ya uongozi wake

Ni bahati mbaya sana jambo hili limeanza kuwa na athari hata kwa timu ya Taifa. Mwamko wa Wanayanga kuiunga mkono timu ya Taifa unazidi kwenda chini

Leo imeundwa Kamati ya ushindi Stars ikiwajumuisha Rais wa GSM Ghalib Said Mohammed akiwa Mwenyekiti huku Injinia Hersi Said akiwa Katibu Mkuu

Kamati hiyo ni kama inatumika 'kuwalainisha' mashabiki wa Yanga waweke silaha chini, waiunge mkono timu yao ya Taifa kupitia viongozi wao wanaowaheshimu sana

Kazi iliyofanywa na GSM ndani ya Yanga inafahamika, Ghalib na Injinia Hersi wamejijengea heshima ya kipekee miongoni mwa mashabiki wa Yanga

Lakini hoja ya msingi hapa ni kwa nini tumefika hapa? kwani timu ya Taifa ni ya Watanzania wote, katika hali ya kawaida mwananchi hahitaji hamasa ili kuiunge mkono timu yake ya Taifa. Ukiona tumefika hapa basi fahamu kuna tatizo mahali

Sawa, kuundwa kwa Kamati ni jambo jema kwani itawahamasisha mashabiki, lakini muhimu zaidi ni kwa TFF kuhakikisha inarekebisha yale mapungufu yanayopelekea baadhi ya mashabiki wasione fahari kuiunga mkono timu yao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’