Misimu ya 2014/15, 2015/16 na 2016/17 ni misimu ambayo kumbukumbu yake imebakia miyoni mwa Wanayanga kutokana na ubora wa kikosi walichokuwa nacho wakati huo
Kikosi cha Yanga katika misimu hiyo kilikuwa hatari. Haikushangaza wababe hao 'kusepa' na taji la ligi kuu kwa misimu mitatu mfululizo
Msimu wa 2015/16 Yanga ilibeba mataji yote katika michuano ya ndani waliyoshiriki lakini pia timu ikafanikiwa kutinga hatua ya makundi michuano ya kombe la Shirikisho
Ni wakati ambao Wanayanga walifurahia na hata sasa wengi wanatamani kuona timu inarejea katika nyakati zile
Yanga ya msimu huu imesukwa upya, dalili njema zimeanza kuonekana mapema. Kwani licha ya timu kutokuwa pamoja kwa muda mrefu tena chini ya mbinu za Krmpotic, timu imepata mafanikio
Ushindi mechi nne za ligi na sare moja, ushindi mechi zote tatu za kirafiki, ni mwanzo mzuri
Ujio wa Cedric Kaze ambaye anatajwa kuwa muumini wa soka la kushambulia, pengine unaweza kuirudisha Yanga zama zile ambazo kila aliyekutana na Yanga alipigwa