Katika kipindi cha siku chache zilizopita kuna video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara akisikika akisema kuwa timu yao haiwezi kupata ushindi kwenye mchezo wowote dhidi ya Yanga ambao utapigwa katika tarehe yoyote yenye namba nane
Sasa baada ya Bodi ya Ligi kutangaza kusogeza mbele mchezo kati ya Yanga na Simba uliokuwa umepangwa kupigwa Oktoba 18, inaweza kutafsiriwa kuwa Simba wameomba tarehe ya mchezo huo ibadilishwe kwa kuhofia kile kilichoelezwa na Manara katika mahojiano yake na Azam TV siku za nyuma
Afisa Habari wa zamani wa klabu ya Yanga Dismas Ten amewapiga 'dongo' wSimba wameenda kuipigia magoti TFF ibadili tarehe hiyo wakihofia kipigo kama alivyotabiri msemaji wao
"Yaani kama siyo 7 tulikuwa tunapiga 10 mnabahati sana mmerudisha mpira kwa kipa...! Mmeoooomba..!, mmefurahi kweli mechi kuahirishwa kisa tarehe ina namba nane," aliandika Ten kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Uamuzi wa Bodi ya Ligi kusogeza mchezo huo mpaka Novemba 07, umewashangaza wengi kwani wakati mchezo huo ukiahirishwa timu nyingine zikiwemo Azam Fc na Namungo Fc ambazo zinao nyota wa kigeni walioitwa timu za Taifa, michezo yao haikuahirishwa
Azam Fc itashuka dimba Oktoba 15 kumenyana na Mwadui Fc wakati mchezo wa Yanga na Simba ulikuwa Oktoba 18!