Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajiwa kukutana Oktoba 12 kujadili madai ya Yanga kuhusu mkataba wa Bernard Morrsion na klabu ya Simba
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Elias Mwanjala amesema wamepanga kukutana Oktoba 12 kujadili madai hayo akiwataka wadau wa soka nchini wasubiri nini kitaamuliwa kwenye kikao hicho
Mapema wiki hii Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alieleza kuwa mkataba wa Morrison na Simba una mapungufu kwani hauna saini ya kiongozi yeyote wa klabu ya Simba
Ni mapungufu kama hayo ambayo yalitumika kubatilisha mkataba wa Mghana huyo aliosaini na klabu ya Yanga na Kamati ya Sheria kumtangaza kuwa mchezaji huru
Β
ADVERTISE HERE