FT : Yanga 3-0 Coastal Union

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2020
FT : Yanga 3-0 Coastal Union

Mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga wametakata uwanja wa Benjamin Mkapa leo wakifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union

Yanga iliuanza mchezo huo taratibu kwenye kipindi cha kwanza, wakiwapa nafasi Coastal Union kutawala kwa muda mwingi

Mabadiliko yaliyofanywa wakati wa mapumziko kwa kuwaingiza Haruna Niyonzima na Deus Kaseke kuchukua nafasi za Zawadi Mauya na Kibwana Shomari yalibadili kabisa taswira ya kikosi cha Yanga

Carlinhos fundi huyu kutoka kule Angola ndiye aliyefungua ukurasa wa mabao leo akiweka kambani bao mahiri kwa kichwa akiunganisha krosi ya Tuisila Kisinda

Haruna Niyonzima 'Baba mzazi' akadhihirisha umuhimu wake kwenye kikosi cha kwanza akiweka kambani bao la pili kwa shuti kali akiitendea haki krosi ya Tuisila Kisinda ambaye aliwachachafya walinzi wa Coastal Union upande wa kushoto

Ulikuwa mpira wa kiwango cha juu uliopigwa ya Yanga katika kipindi cha pili wakiwaacha Coastal Union wasiamini kile walichokuwa wakikishuhudia

Katika dakika ya 64 Yacouba Sogne akafungua akaunti yake ya mabao akiweka kambani bao la tatu akimalizia pasi mpenyezo iliyopigwa na Mukoko Tonombe

Sogne angeweza kuondoka na mpira leo kama ungeweza kutumia nafasi nyingine alizotengenezewa

Kwa ufupi, kiwango kilichoonyeshwa na Yanga kwenye kipindi cha pili ni salamu tosha kwa wale waliokuwa wakiibeza Yanga

Ni wazi Yanga iko kwenye mwelekeo sahihi, ule msemo wa kocha msaidizi Juma Mwambusi kuwa kuna timu zitakuja kupigwa bao nane, dalili zinaanza kuonekana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’