Kikosi cha Yanga usiku wa leo majira ya saa moja kitashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuumana na Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom, raundi ya tano
Baada ya kushinda mechi zote mbili zilizopita mikoani, Yanga inarejea nyumbani kuendeleza msako wa alama tatu
Ni kwa kiingilio cha Mzunguko Tsh 5,000, VIP B&C Tsh 10,000 na VIP A Tsh 15,000. Tiketi zilianza kuuzwa tangu jana ambapo mashabiki wameaswa kununua tiketi mapema katika vituo vilivyotangazwa ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza uwanjani
Wenyewe Wananchi wanasema leo ndio wanaanza ligi hivyo burudani kabambe inasubiriwa kutoka kwa mabingwa hao wa kihistoria
Ni kuanzia saa moja kamili usiku
ADVERTISE HERE