Ligi Kuu ya Vodacom leo imeingia mzunguuko wa nne kwa mechi mbili kupigwa kule mkoani Kagera na Mbeya
Kagera Sugar imezinduka kutoka usingizini baada ya kufanikiwa kuwalaza vinara wa ligi hiyo KMC kwa bao 1-0
Nyota zao la klabu ya Yanga Yusuf Mhilu ndiye aliyeifungia Kagera Sugar bao la ushindi
Mbeya City imeendelea na mwenendo wa kugawa pointi baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Namungo Fc
Mbeya City sasa imekamilisha michezo minne bila ya kuambulia pointi wala kufunga bao
Ligi hiyo itaendelea kesho Jumamosi kwa mechi nyingine tatu kupigwa wakati Yanga ikitarajiwa kushuka dimbani keshokutwa kuumana na Mtibwa Sugar mkoani Morogoro
ADVERTISE HERE