Mtibwa Sugar hawatatoka salama Jumapili - Niyonzima

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Sep 2020
Mtibwa Sugar hawatatoka salama Jumapili - Niyonzima

Wachezaji wa Yanga wamepania kuendeleza wimbi wa ushindi pale watakapochuana na Mtibwa Sugar kule mkoani Morogoro Jumapili

Nahodha Msaidizi wa mabingwa hao wa kihistoria Haruna Niyonzima, amesema malengo ya timu ni kuhakikisha wanashinda kila mchezo watakaocheza bila ya kujali wako nyumbani au ugenini

Yanga iliingia kambini jana mchana kujiandaa na mchezo huo watakaocheza Uwanja wa Jamhuri.

Timu hiyo iliyo chini ya kocha, Zlatko Krmpotic, itakwenda mkoani Morogoro katika mchezo wake wa pili ugenini baada ya awali kukipiga na Kagera Sugar, mjini Bukoba, Kagera na kutoka na ushindi wa bao 1-0.

Niyonzima amesema pamoja na kutambua ubora wa kikosi cha Mtibwa Sugar, lakini wanahitaji matokeo ili kuhakikisha wanatimiza malengo waliyoweka msimu huu

"Tunafahamu Mtibwa Sugar ni timu nzuri, mara nyingi wanapocheza uwanja wao wa nyumbani huwa sio wepesi, lakini tumejipanga"

"Tunahitaji kuvuna alama zote tatu bila ya kujali tunacheza na timu ipi au uwanja gani tunatumia, tutakwenda kupambana na kurejea nyumbani tukiwa na kile tunachohitaji," alisema.

Katika misimu miwili iliyopita Yanga ilishindwa kuondoka alama zote tatu katika mechi walizocheza na Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri

Mwaka juzi walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na msimu uliopita wakatoka sare ya bao 1-1

Mchezo wa Jumapili unatarajiwa kuwa na ushindani mkali, utapigwa katika mazingira ya uwanja ambao mara nyingi umelalamikiwa kuwa sio rafiki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’