Benki ya KCB imeingia mkataba na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) wa udhamini wa ligi kuu ya Vodacom wenye thamani ya shilingi milioni 500 kwa muda wa mwaka mmoja.
Huu ni mwaka wa nne mfululizo kwa KCB inadhamini ligi kuu ili kuchangia maendeleo ya soka la Tanzania ambalo limeanza kufanya vizuri.
Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa KCB, Barry Chale amesema dhamira yao nikurudisha kwa jamii kupitia kwenye Michezo kwakua ni sekta inayotoa ajira kwa vijana wengi nchini.
"Leo tumeingia mkataba wa mwaka mmoja na TFF kwa ajili ya udhamini wa ligi kuu wenye thamani ya shilingi milioni 500. Tunafanya kazi na TFF huu ni mwaka nne ushirikiano tunaopata ni mkubwa na tuna imani tutaendelea kufanya nao kazi kwa miaka mingine ijayo," amesema Barry.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ligi Steven Mguto ambaye alimuwakilisha Rais wa TFF ameishukuru KCB kwa udhamini huo ambao utakuwa ni msaada mkubwa kwa klabu shiriki.