Stars hiyooo nusu fainali ya Cosafa

Admin By Admin
β€’
3 Jul 2017
Stars hiyooo nusu fainali ya Cosafa
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imetinga nusu fainali ya michuano ya Cosafa baada ya kuilaza Afrika Kusini bao 1-0.

Afrika Kusini ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo na wameaga mashindano yanayofanyika kwenye ardhi yao.

Elius Maguri aliyekuwa nyota wa mchezo, alifunga bao pekee la Stars kwenye dakika ya 22 kipindi cha kwanza baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Afrika Kusini wliodhani alikuwa ameotea.

Safu ya Ulinzi ya Stars iliyokuwa chini ya Erasto Nyoni na Salim Bonde pamoja na mlinda lango Aishi Manula wanastahili pongezi za kipekee kwani licha ya Stars kuwa inashambuliwa na Afrika Kusini kwa muda mrefu, uimara wao ulisaidia Stars kutoruhusu bao.

Afrika Kusini ikitumia kikosi cha vijana ilitawala mchezo huo kwa zaidi ya asilimia 60 lakini walikosa mbinu ya kupenyeza mipira ya mwisho.

Stars ambayo ni waalikwa katika michuano hiyo sasa itachuana na Zambia katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa Jumatano ijayo.

Teamsl

Bafana: Pule, Mukumela, Maela, Gordinho, Booysen, Masalesa, Alexander, Norodien (Maboe 78Ò€ℒ), Webber, Jordan (Mokate 60Ò€ℒ), Moseamedi

Unused subs: Johnson, Bvuma, Malepe, Mvala, Sibiya, Mthethwa, Mbatha

Tanzania: Manula, Gadiel, Nyoni, Mbonde, Mkami, Maguri, Ulimwengu, Daudi Raphael, Shizza, Yasin Said, Kapombe
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’