Hatimaye shehena ya jezi za klabu ya Yanga zimewasili kutoka huko Uchina. Wakati wowote GSM kwa kushirikiana na uongozi wa Yanga watazitambulisha jezi hizo na kuweka hadharani utaratibu wa upatikanaji wake
Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amewataka mashabiki wa timu hiyo sasa wajiandae kuupokea uzi bora zaidi nchini baada ya kuusubiri kwa miezi kadhaa
Msimu huu Yanga itakuwa na jezi za aina tatu, jezi ya nyumbani itakayokuwa na rangi ya kijani, jezi ya ugenini pamoja na ile ya dharura zitakuwa na rangi za njano na nyeusi
Sasa wananchi mnaweza kupumua, mzigo umeshatua, huu hapa..!

ADVERTISE HERE