Msimu huu ni wetu - Dk Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Sep 2020
Msimu huu ni wetu - Dk Msolla

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amewahakikishia wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa msimu huu utakuwa wa furaha kwao kutokana na usajili uliofanyika

Pia, Dk Msolla ameishukuru kampuni ya GSM kwa kufanikisha usajili wa wachezaji wazuri hasa wale watano wa kigeni ambao viwango vyao ni hadhi ya Kimataifa

Amesema baada ya kuwashuhudia nyota hao wakicheza kwa mara ya kwanza, pamoja na usajili makini wa wazawa, ana uhakika msimu huu utakuwa wa mafanikio kwa Yanga

"Usajili uliofanyika ni mkubwa sana, nakiri, tangu niingie kwenye uongozi wa Yanga, safari hii tuna kikosi ambacho kitarudisha heshima ya klabu yetu," Dk Msolla alinukuliwa na Mwanaspoti

"Angalia uwezo wa nyota wa kigeni walioonyesha kwenye mchezo wao wa kwanza tu, ni wachezaji bora sana ambao wana kiu ya kutaka kuisaidia Yanga kuweza kufikia malengo yake"

Aidha Dk Msolla amewataka mashabiki wa Yanga kuwa watulivu wakati benchi la ufundi likiendelea kuwaunganisha wachezaji

"Kutokana na usajili mkubwa tuliofanya, sasa ni kama tuna timu mpya, kocha alihitaji angalau siku 10 hadi 15 kuweza kuandaa timu, nadhani tumpe muda. Tumepata makocha wazuri lakini wamekutana na kikosi ambacho ni kipya na kwa bahati mbaya walichelewa kuanza majukumu yao"

Dk Msolla ambaye kitaalamu ni kocha, amesema anatarajia ushindani mkali wa namba kwenye kikosi cha msimu huu kutokana na ubora wa wachezaji

Anaamini ushindani huo utasaidia wachezaji kujituma zaidi ili kuhakikisha wanapata nafasi endelevu kwenye kikosi cha kwanza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’