Mshambuliaji wa Yanga Yacouba Songne amefanya mazoezi na kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria kwa takribani siku nne, yuko tayari kuwakabili Tanzania Prisons leo
Hata hivyo hatma ya kuanzishwa au la inabaki mikononi mwa kocha mkuu Zlatiko Krmpotic kama ameridhishwa na utimamu wake wa mwili 'fitnes' baada ya siku alizofanya mazoezi na wenzake
Zlatko leo anaweza kuwa na wakati mgumu kuamua aanze na nani kwani vijana wote wako 'moto' kwelikweli
Pengine tunaweza kukishuhudia kikosi kilichoanza mchezo dhidi ya Aigle Noir wiki iliyopita, kikiwa na mabadiliko machache tu
Muhimu kwa Yanga leo ni kuhakikisha wanaanza msimu kwa kukusanya alama zote tatu
Ushindi ndio matokeo ambayo kila Mwanayanga anayasubiri pamoja na kuwa mpira una matokeo ya aina tatu