Chuji anastaafu leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Aug 2020
Chuji anastaafu leo

Kiungo mahiri aliyejizolea sifa kemkem wakati akiitumikia klabu ya Yanga Athumani Idd Chuji, anastaafu kucheza soka leo

Chuji atatumia siku ya Wananchi leo kustaafu soka, atakuwepo dimbani katika moja ya mechi za utangulizi zitazowahusisha wakongwe wa Yanga

Huyu ni mmoja wa wachezaji ambao Yanga inajivunia katika kipindi cha miaka 10 iliyopita

Alikuwa fundi kwelikweli, wale ambao hawakubahatika kumuona wakati akiwa bado kijana na kwenye ubora wake, hakika wamekosa burudani sana

Huyu ndiye Chuji ambaye alikuwa fundi wa zile pasi za kuhamisha uwanja, shukrani kwa Yanga kumleta Carlinhos kwani atawakumbusha Wananchi enzi za mwamba huyu

Chuji amestahili kustaafu kwa heshima, kwani amefanya mambo makubwa kwa nchi hii, sio kwa klabu ya Yanga pekee, amecheza timu ya taifa kwa mafanikio pia

Lakini amewahi kuzitumikia Simba na Azam Fc kwa vipindi tofauti

Amepewa heshima kuitumia siku ya leo kutundika daruga, ni heshima aliyostahili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
58m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’