Tuko tayari kuikabili Aigle Noir - Bumbuli

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Aug 2020
Tuko tayari kuikabili Aigle Noir - Bumbuli

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kikosi chao kiko tayari kwa mchezo wa kilele cha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Aigle Noir ambao utapigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Mkapa

Akizungumza na Wanahabari akiwa sambamba na Msemaji wa Aigle Noir, Bumbuli amesema wamejipanga kuwapa burudani mashabiki wao katika mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa moja jioni

"Vijana wako vizuri, wako tayari kuwapa furaha mashabiki. Tumefanya usajili mkubwa, tuna kikosi ghali ambacho kimetugharimu zaidi ya Bilioni 2.5. Tunawatahadharisha tu wapinzani wetu wajiandae kwani wanaenda kukutana na timu imara sana"

"Wanaenda kukutana na timu ambayo msimu ujao ina malengo ya kutwaa ubingwa wa Afrika," alitamba Bumbuli

"Leo jioni tutafanya mazoezi kwenye uwanja wa Mkapa kwa muda wa saa moja kuanzia saa 10, kisha tutawapa nafasi wageni wetu Aigle Noir wafanye mazoezi kuanzia saa 11"

Aidha Bumbuli amewataka mashabiki wachangamkie tiketi kwani mpaka sasa baadhi ya tiketi zimekwisha

"Tiketi za Royal zimemalizika, VIP A nazo ziko mbioni kumalizika na hata VIP B na C. Hivyo kwa wale mashabiki ambao hawajajipatia tiketi wanashauriwa waharakishe" alisema

Nae msemaji wa Aigle Noir, ametamba kuwa timu yao imekuja kushindana na Yanga hivyo mashabiki watarajie burudani nzuri kutoka kwao

"Timu yetu ina wachezaji kutoka DR Congo, Ivory Coast na hata hapa Tanzania. Tunajua ni mchezo wa kirafiki, mchezo wa ujirani mwema lakini tunafahamu mashabiki wanataka burudani, tuko tayari," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’