Kiungo mpya wa Yanga Carlos Fernandes 'Carlinhos' ameanza rasmi mazoezi na wenzake yakiwa maandalizi kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi siku ya Jumapili, August 30 2020
Carlinhos aliyetua juzi kutoka Angola na kuvunja rekodi kwa kupokewa na idadi kubwa ya mashabiki, jana alipewa mazoezi ya peke yake na kocha Juma Mwambusi
Fundi huyo wa mpira leo amejumuishwa na wachezaji wengine ambao walianza mazoezi mapema
Yanga inafanya mazoezi yake katika uwanja wa chuo cha Sheria, Ubungo jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa kilele cha Wiki ya Mwananchi dhidi ya Aigle Noir utakaopigwa Jumapili
Kocha Mwambusi ameanza kusimamia program za Mazoezi tangu jana akishirikiana na kocha wa viungo Riedoh Berdien
ADVERTISE HERE