Kiungo mpya wa Yanga Carlos Fernandes 'Carlinhos' amefichua kuwa alipofika uwanja wa Ndege wa Adis Ababa akiwa safarini kuja nchini, walijitokeza watu waliojitambulisha kuwa maafisa wa klabu ya Yanga kuwa wametumwa kumpokea
Carlinhos amesema kwa kuwa alikuwa akifanya mawasiliano na viongozi wa Yanga pamoja na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said, aliwakatalia kwani hawakuwa miongoni mwa viongozi wa Yanga aliokuwa akiwasiliana nao
Hata alipotua JNIA, kulikuwa na jaribio jingine la kumteka, lakini halikufanikiwa
"Kuna watu walinifuata Ethiopia nikiwa njiani kuja Tanzania na kujitambulisha kuwa wao ni Yanga wamenifuata kunipokea lakini nilikataa! Nawajua viongozi wangu kwa sura na nilikuwa nawasiliana nao hivyo hawakuweza kunihadaa," alisema Carlinhos baada ya kumwaga wino wa kuitumikia Yanga kwa miaka miwili
Kwa miaka ya karibuni Simba imesajili wachezaji wengi kupitai mgongo wa Yanga. Pengine sakata la Morrison limeifanya Yanga iongeze umakini na sasa haitakuwa rahisi tena 'kukwapua' wachezaji wa Yanga
Β