Dk Msolla amkaribisha Carlinhos Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Aug 2020
Dk Msolla amkaribisha Carlinhos Yanga

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla amempokea Makao Makuu ya klabu kiungo fundi Carlos Fernandos maarufu Carlinhos

Mwamba huyo kutoka nchini Angola amepokelewa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na Maelefu ya Mashabiki wa klabu ya Yanga

Akiongozana na Injinia Hersi said na waandamizi wengine, Carlinhos alisindikizwa na nyomi la mashabiki mpaka Jangwani yalipo Makao Makuu ya Yanga ambako alipokelewa na Dk Msolla na kisha kukabidhiwa jezi ya Yanga ikiwa ishara kuwa amefika katika mikono salama ya mabingwa hao wa kihistoria

Gumzo kubwa ni idadi ya mashabiki waliojitokeza kumpokea fundi huyo, hakika Yanga inadhihirisha kuwa klabu pendwa zaidi hapa nchini

Matukio haya ya kipekee ya mapokezi ya nyota wapya, ni ujumbe muhimu kwa wachezaji hao kuwa matumaini ya Wanayanga wengi yako mikononi

Naamini nyota hawa hawakuwahi kukutana na mapokezi ya kishindo ya namna hii katika nchi walizokuwa wakicheza awali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’