Baada ya Mkutano na Wanahabari utakaofanyika saa sita mchana, Wanachama na Mashabiki wa Yanga wataelekea uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kumpokea kiungo mpya wa mabingwa hao wa kihistoria Carlos Fernandes 'Carlinhos' anayetua kutoka kule Angola
Kama ilivyokuwa kwa mapokezi ya Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe, leo Wanayanga wanatarajia kufunga mitaa katika mapokezi ya fundi huyo wa mpira
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema mapokezi ya Carlinhos ni sehemu ya shamra shamra kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi siku ya Jumapili, August 30 2020
Carlinhos amezungumzwa sana tangu wiki iliyopita, kwa hakika ujio wake utatetemesha jiji la Dar es salaam
ADVERTISE HERE