Uongozi wa klabu ya Rayon Sports umethibitisha kupokea Mwaliko kutoka kwa klabu ya Yanga kuwakaribisha katika tukio la kilele cha wiki ya Mwananchi ambalo litafanyika mwishoni wa mwezi huu
Kesho Yanga itazindua rasmi shamrashamra za wiki ya Mwananchi kule mkoani Dodoma na pengine Rayon Sports ambao walikuwa wakisubiriwa wathibitishe ushiriki wao, wanaweza kutangazwa kuja kucheza na Yanga wiki ya Mwananchi mwishoni mwa wiki ijayo
Akizungumza baada ya mazoezi ya leo asubuhi, mlinda lango wa Yanga Farouk Shikhalo amesema wamejipanga kuwapa furaha mashabiki na kuwa watatumia mchezo wa wiki ya Mwananchi kudhihirisha dhamira yao kurejesha heshima ya Yanga msimu ujao
Kikosi cha Yanga kinaendelea kujifua chini ya kocha Riedoh Berdien ambaye anatimiza majukumu yake kwa ushirikiano wa kocha mkuu anayesubiri kutangazwa na uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria