Jana baada ya kuwasili kutoka DR Congo, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, alisema wanawasubiri wachezaji wengine watatu wa kigeni kufunga hesabu za usajili
Mshambuliaji Yacouba Sogne yeye tayari anafahamika na anaweza kuwasili mwishoni mwa wiki hii
Lakini mapema jana Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela akabainisha ujio aliyekuwa mshambuliaji wa Rayon Sports Michael Sarpong na kiungo fundi sana Carlinhos anayetokea Interclube ya Angola
Imeelezwa Sarpong anaweza kutua leo wakati Carlinhos akisubiriwa mwishoni mwa wiki
ADVERTISE HERE