Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Yikpe Gnamien amemalizana na uongozi wa timu hiyo baada ya makubaliano ya kuvunjwa mkataba wake kufikiwa
Yikpe alitua Yanga mwezi Januari usajili wa dirisha dogo akitokea klabu ya Gor Mahia
Ni mmoja wa wachezaji waliokuwa katika presha kubwa kutoka kwa mashabiki waliokuwa hawakubali uwezo wake
Miezi sita aliyoitumikia Yanga aliweza kufunga mabao matatu, mawili kwenye ligi na moja kwenye kombe la FA
"Tunakutakia kila la kheri, tunakushukuru kwa kuwa sehemu ya historia yetu, mchango wako tutaendelea kuuthamini," salamu za shukrani kwake zilizotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick
ADVERTISE HERE