Ligi ya Mabingwa yanukia Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Aug 2020
Ligi ya Mabingwa yanukia Yanga

Kinachosubiriwa sasa ni taarifa rasmi kutoka kwa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) juu ya hatma ya Yanga kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu unaoanza mwezi ujao

Lakini dalili njema zimeonekana baada ya CAF kuthibitisha kuiondoa Libya katika michuano hiyo baada ya kukosa sifa

Serikali ya Libya ilisitisha shughuli zote za michezo kuanzia msimu uliopita kutokana na vita inayoendelea nchini humo

Libya ilipaswa kutoa nafasi nne kwenye michuano ya CAF baada ya kushika nafasi ya 12 ambayo ni ya mwisho katika zile nchi zinazopaswa kutoa timu nne

Tanzania inashika nafasi ya 13 hivyo ni wazi itachukua nafasi ya Libya ambayo imeondolewa baada ya kutoendesha ligi huu ukiwa msimu wa pili

Lakini pia nchi za Ethiopia, Afrika ya Kati na Sudan Kusini nazo hazijatoa Wawakilishi baada ya kufuta ligi zao mapema kutokana na janga la corona

Yanga imeaswa kufanya maandalizi ya michuano hiyo kwani ikitokeaTanzania imeongezewa nafasi, muda wa maandalizi unaweza kuwa mdogo kama ilivyokuwa msimu uliopita

 

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’