Senzo kapewa majukumu haya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Aug 2020
Senzo kapewa majukumu haya Yanga

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Senzo Mazingisa ambaye mapema wiki hii GSM waliifanyia Simba 'umafya' kwa kumchukua mchana kweupee, anatarajiwa kuwa mshauri mkuu wa uongozi wa Yanga katika masuala mbalimbali

Kwa sasa Katiba ya Yanga hairuhusu raia wa kigeni kuwa Mtendaji Mkuu (Katibu) , Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema kwa wakati huu Senzo atakuwa mshauri wa uongozi katika masuala mbalimbali

Miongoni mwa majukumu mengine ambayo Senzo atafanya ndani ya uongozi wa Yanga ni pamoja na kutoa mwongozo wa uwajibikaji wa idara zote, kupanga bajeti za klabu pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato

Senzo atasimamia weledi katika masuala yote yatakayokuwa yakifanyika ndani ya klabu ya Yanga

Pia atakuwa na mchango katika mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ambao awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika August 30

Senzo raia wa Afrika Kusini ana uzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi wa soka, akiwa amewahi kuwa Mtendaji wa vilabu vya Orlando Pirates na Platinum Stars huko Afrika Kusini kabla ya kuja nchini kujiunga na Simba

Lakini pia alikuwa sehemu ya jopo la wataalamu wa Kamati iliyosimamia maandalizi ya michuano ya kombe la dunia iliyofanyika Afrika Kusini mwaka 2010

Hivyo ujio wake Yanga mwafaka wakati huu mabingwa hao wa kihistoria wakijipanga kupiga hatua nyingine ambayo itaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’