Uongozi wa klabu ya Yanga umesema unajipanga kupeleka ofa ya tatu kunako klabu ya Azam Fc ili kumsajili kiungo Salum Abubakar Sure Boy
Yanga tayari imewasilisha ofa mbili kwa Azam Fc ambao wamegoma kumuuza wakitaka fedha zaidi licha ya mchezaji mwenyewe kuomba aachwe akajiunge na Yanga
Sureboy ana mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Azam Fc
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema watajaribu mara ya tatu kumsajili mchezaji huyo
"Bado hatujakata tamaa kumsajili Sure Boy licha ya kukataliwa ofa ya kwanza na ya pili ila tunajipanga kupeleka ofa ya tatu na iliyobora zaidi na naamini kwakuwa Sure Boy mwenyewe alishaonyesha nia kutua Yanga basi tutapambana mpaka mwisho," alisema Bumbuli kwenye mahojiano na Wasafi Radio
Yanga inakamilisha kamilisha usajili wa nyota wa ndani kabla ya kuanza kupokea maproo ambao imeelezwa mpaka kufikia Jumamosi wote watakuwa wamewasili