Baada ya kikao kizito cha viongozi wa klabu Yanga, inalezwa kuwa mabingwa hao wa kihistoria wamefikia uamuzi wa kumpa timu Patrick Aussems na atatua nchini muda wowote ndani ya wiki hii
Aussems alipata mafanikio makubwa alipokuwa na Simba kwa kuisaidia timu hiyo kucheza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa mwaka juzi
Huyu ni kocha anayelifahamu vizuri soka la Tanzania, tetesi za ujio wake zilivuja jana jioni wakati wa sekeseke la kumpokea aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa
Yanga inakimbizana na muda kuweka sawa benchi lake la ufundi kabla ya mikiki mikiki ya ligi kuanza Septemba 06
Hafidh arejeshwa
Katika hatua nyingine, aliyewahi kuwa Meneja wa Yanga Hafidh Seleh, amerejeshwa katika nafasi hiyo
Hafidh aliondolewa mwishoni mwa mwaka uliopita wakati Yanga ilipovunja benchi la ufundi lililokuwa chini ya kocha Mwinyi Zahera
Kabla ya kuondolewa, Hafidh alidumu kwenye nafasi hiyo kwa zaidi ya misimu mitano