Kimeeleweka bila Tshishimbi, Kamusoko, Tambwe na Ngoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Nov 2017
Kimeeleweka bila Tshishimbi, Kamusoko, Tambwe na Ngoma
Wapo waliokuwa wamekata tamaa pale kikosi cha Yanga kilichoshuka dimbani dhidi ya Mbeya City kilipowekwa hadharani.

Hawa waliamini kwa kutoyaona majina ya wakali Kelvin Yondani, Papi Tshishimbi, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe na Donaldo Ngoma kwenye kikosi basi Yanga ingechapwa.

Japo wangekuwepo 'INGEPENDEZA ZAIDI' lakini vijana waliopewa nafasi leo wamedhihirisha msimu huu Yanga haitegemei mchezaji mmoja kwani wamefanya kazi sawasawa ilivyotakiwa.

Tshishimbi alikumbwa na malaria kabla hajapata majeraha madogo siku moja kabla ya mchezo huku Kamusoko, Tambwe na Ngoma sote tukiwa tunafahamu bado ni majeruhi.

Hata hivyo wachezaji waliopata nafasi leo wamewapa POLE na kuwatakia kheri wapone haraka kwani bila ya hivyo wanaweza wakarejea na kujikuta wanasugua benchi.

Leo tumemshuhudia nahodha Cannavaro akiwa kwenye ubora wake na kuifanya ipasavyo kazi tuliyozoea kuona inafanywa na kelvin Yondani.

Utu uzima dawa! Mkongwe Cannavaro bado yupo sana Yanga.

Pato Ngonyani, Raphael Daudi na Ibrahim Ajib walinoga kwelikweli pale katikati. Pasi zao za mwisho nusura ziwatoe roho walinzi wa Mbeya City.

Emanuel Martin, Obrey Chirwa na Pius Buswita walikuwa moto wa kuotea mbali!

Kwa ujumla kasi ya ushambuliaji ya Yanga ilivutia sana.

Kocha George Lwandamina anastahili pongezi za dhati kwa kuweza kutengeneza kikosi imara ambacho kwa mwenendo huu kinaenda kutwaa ubingwa wa nne mfululizo.

Tayari matumaini ya Yanga inayoweza kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa yameanza kuonekana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’