Aliyekuwa nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi ni kama ameweka silaha chini baada ya kuwasiliana na viongozi wa Yanga akiomba apewe mkataba asaini
Yanga ilitangaza kuachana na Tshishimbi baada ya kuhitaji kuongezwa dau la usajili kinyume na makubaliano ya awali
Inaelezwa Tshishimbi ameonyesha utayari wa kusaini mkataba kwa makubaliano ya awali
"Tshishimbi ameomba apewe mkataba asaini ili aendelee kubaki hapa. Yuko tayari kusaini mkataba kwa makubaliano ya awali," alifichua mtoa taarifa
Juzi baada ya Yanga kutangaza kuachana nae, Tshishimbi alieleza kushitushwa na uamuzi huo ambao hakuutarajia
Wakati yuko kwenye mazungumzo na Yanga alidai kuwa na ofa nono kutoka klabu ya Simba lakini baada ya Yanga kutangaza kumtema, timu hiyo haionekani kumfuatilia
Hata Azam Fc nayo tayari imeshasajili kiungo mkabaji hivyo kumuacha Mcongomani huyo asijue cha kufanya
Kama Yanga itaamua kumfungia 'vioo' huenda akalazimika kurejea kwao DR Congo kama hatapata ofa hapa nchini