Yanga yajipanga kuanza mazoezi mapema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Aug 2020
Yanga yajipanga kuanza mazoezi mapema

Baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuweka hadharani kalenda ya msimu ujao ligi kuu ya Vodacom ikitarajiwa kuanza Septemba 06 2020, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuanza maandalizi ya msimu mpya wiki ijayo, August 10 imefahamika

Mabingwa hao wa kihistoria kwa sasa wanakamilisha michakato ya usajili lakini wakipanga kulikamilisha zoezi hilo kabla ya timu kuanza mazoezi

Aidha, mtoa taarifa amebainisha kuwa jana mabosi wa Yanga walikutana kupitia barua 64 za maombi ya nafasi ya Kocha Mkuu ambaye anatarajiwa kurithi mikoba  ya Luc Eymael aliyetimuliwa wiki iliyopita

Yanga imedhamiria kuanza mazoezi ikiwa tayari na kocha mkuu hivyo mpaka kufikia mwishoni mwa wiki, kocha huyo atakuwa amefahamika

Mabingwa hao wa kihistoria watakuwa na takribani siku 26 kujifua tayari kwa mikiki mikiki ya ligi ambayo wamepania kutwaa ubingwa walioukosa kwa misimu mitatu mfululizo

Lakini pia, kabla ya ligi Yanga itakuwa na tukio kubwa la wiki ya Mwananchi ambalo bado tarehe yake haijawekwa hadharani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’