Kagera Sugar wamkomalia Mhilu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Aug 2020
Kagera Sugar wamkomalia Mhilu

Pamoja na wengi kutamani kumuona mshambuliaji Yusufu Mhilu akirejea 'nyumbani', jambo hilo halionekani kukamilika baada ya Kagera Sugar kufanikiwa kumuongezea mkataba

Katibu Mkuu wa Kagera Sugar Ally Said amesema Mhilu ni miongoni mwa wachezaji waliofanikiwa kuwaongeza mikataba na atakuwa na wakata miwa hao kwa misimu mingine miwili

Tayari Yanga imeweza kumn'goa kiungo mkabaji Zawadi Mauya kutoka klabu hiyo ya Kagera Sugar

Kwa nyakati tofauti ilihusishwa kutaka kumrejesha Mhilu, aliyelelewa Yanga B kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza na Hans van Pluijm wakati huo akiwa kocha mkuu wa Yanga

Hata hivyo, mwezi Januari mwaka 2019 Yanga ilimtoa Mhilu kwa mkopo kwenda klabu ya Ndanda Fc kabla ya kujiunga na Kagera Sugar kwa mkataba wa mwaka mmoja katika dirisha la usajili la msimu uliomalizika

Yanga imemsajili mshambuliaji mzawa Waziri Junior, na pengine kuachana na mpango wa kumsajili Mhilu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’