Msimu umekwisha, tujipange kwa msimu ujao

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
26 Jul 2020
Msimu umekwisha, tujipange kwa msimu ujao

Pamoja na changamoto nyingi msimu huu, Yanga imefunga msimu 'kibabe' kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli Fc na kujihakikishia kumaliza katika nafasi ya pili

Msimu wa 2019-20, ulijaa machungu mengi kwa mashabiki, msimu huu unapaswa kuwa somo kwa mabosi wa Yanga kuhakikisha hawarejei makosa yaliyopelekea timu isiweze kufikia malengo na matarajio ya wengi

Jambo kubwa ambalo kila shabiki anataka kuona ni umakini katika usajili wa wachezaji

Msimu huu uliomalizika Yanga ilisajili wachezaji wapya wanaofika 22,  ni kutokana na makosa yaliyofanywa kwenye usajili wa dirisha kubwa ambapo mabingwa hao wa kihistoria kwa usaidizi wa GSM, walilazimika kufanya usajili mwingine mwezi Januari wakati wa dirisha dogo

Lakini pia kulikuwa na mabadiliko ya benchi la ufundi katikati ya msimu, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa liliathiri muunganiko wa timu

Jambo muhimu zaidi ambalo mabosi wa Yanga wanapaswa kulizingatia ni muda wa maandalizi ya msimu mpya

Msimu huu Yanga haikuwa na maandalizi mazuri. Timu iliweka kambi mkoani Morogoro tena ikinolewa na kocha msaidizi kwa muda mwingi

Pengine michuano ya Afcon 2019 ilichangia kukosekana kwa kocha Mwinyi Zahera, lakini Mcongomani huyo angeweza kurudi mapema kwani timu yake ilitolewa mapema tu kwenye raundi ya kwanza

Kambi nzuri, muda wa kutosha kufanya maandalizi, ni mambo ya msingi ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika maandalizi yajayo

Wanayanga kila mmoja atakuwa makini kufuatilia yanayoendelea pale Jangwani kwani kwa hakika hakuna shabiki ambaye atakuwa tayari kuendelea 'kuugulia' msimu ujao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’