Mmachinga atamba, angefunga mabao 40 ligi ya sasa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jul 2020
Mmachinga atamba, angefunga mabao 40 ligi ya sasa

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, mkongwe Mohammed Hussein 'Mmachinga' amesema soka limekuwa rahisi sana wakati huu kuliko walipokuwa wakicheza wao miaka ya nyuma

Mfumania nyavu huyo anayeshikilia rekodi ya mabao,  amesema kama angekuwa anacheza zama hizi, angeweza kumaliza msimu kwa kufunga zaidi ya mabao 40

Mmachinga ndiye anayeshikilia rekodi ya ufungaji bora wa ligi kuu akipachika mabao 26 msimu wa 1997/98 wakati huo ligi kuu ikishirikisha timu 12 tu

"Nikiwatazama mabeki wa sasa ukilinganisha na wakati wetu, nafikiri ningewepo kwenye kizazi hiki ningemaliza msimu na zaidi ya mabao 40," alitamba Mmachinga

Katika maisha yake yote ya soka, Mmachinga hakuwahi kupiga mkwaju wa penati, amewapa changamoto washambuliaji wazawa kuongeza juhudi kuhakikisha hawazidiwi na wageni

"Washambuliaji wazawa ni kama wamelala kidogo katika misimu ya hivi karibuni, wanapaswa kuongeza juhudi kushindana na wenzao wageni kwani naamini uwezo wanao"

Akizungumzia rekodi yake ya mabao 26 kukaribiwa kuvunjwa na mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere, Mmachinga amesema kama Simba itapata mikwaju ya penati mitano kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Polisi Tanzania basi ataweza kuivunja

"Mimi sikuwahi kupiga mkwaju wa penati, ni jambo ambalo sikuwa nikipendelea kufanya. Kagere ni mchezaji mzuri, anapambana sana anapokuwa uwanjani lakini penati zinachangia mabao mengi anayofunga. Hivyo kama Simba watapata penati tano kwenye mchezo wao wa mwisho, basi ataweza kuivunja"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’