Baada ya mchezo mmoja wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa leo kuishuhudia Singida United ikiilaza Lipuli bao 1-0, michezo kadhaa ya ligi hiyo itapigwa kesho Jumamosi.
Jumamosi, Novemba 18 Tanzania Prisons wataikaribisha Simba kwenye dimba la Sokoine huku Ruvu Shooting watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Stand United na Mwadui FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Maji Maji na Mbao FC Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.
Mzunguko wa 10 utakamilishwa siku ya Jumapili Novemba 19 kwa michezo miwili, Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam, Yanga watakuwa wenyeji wa Mbeya City na Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, wenyeji Njombe Mji FC wataikaribisha Azam FC.
Simba inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 19, sawa na Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao, wakati Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 17, sawa na Mtibwa Sugar na Singida United.

ADVERTISE HERE