Sare ya Yanga inaweza kuwashusha daraja Mtibwa Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jul 2020
Sare ya Yanga inaweza kuwashusha daraja Mtibwa Sugar

Wakati mashabiki wa Yanga wakisikitika kwa timu yao kushindwa kupata ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar, kwa upande wa wakata miwa hao hali ni mbaya zaidi kwani wanaweza kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao

Mtibwa Sugar ilihitaji kupata matokeo ya ushindi tu katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Jamhuri

Matokeo hayo yameifanya Mtibwa Sugar kufikisha pointi 42 katika nafasi ya 14 huku Yanga ikifisha alama 69 tatu mbele ya Azam itakayoshuka dimbani nyumbani leo dhidi ya Mbeya City.

Kama Lipuli Fc itapata ushindi hata sare dhidi ya Ruvu Shooting leo, ni wazi Mtibwa Sugar rasmi itaelekea kwenye shimo la kuteremka daraja

Mtibwa Sugar ni moja ya timu zilizotoa changamoto kwenye ligi katika kipindi cha miaka 20 lakini msimu huu timu hiyo imeshindwa kuonyesha makali yake

Katika mechi ya jana, ni Yanga iliyoanza kwa kasi Yanga ikiwa ya kwanza kuliandama lango la Mtibwa na kupata kona doto dakika ya pili lakini ziligeuka kuwa tasa.

Dakika ya tano na saba Mtibwa ililiandama lango la Yanga na kupata faulo mbili lakini hazikuwa na macho.

Salum Kihimbwa akiwa wingi wa kulia alitumia mabavu na ujanja dhidi ya Juma Makapu na kupiga krosi iliyounganishwa nyavuni na Haruna Chanongo dakika ya 28.

Mtibwa iliendelea kuliandama lango la Yanga ikiongozwa na Kihimbwa ambaye alionekana kuisumbua safu ya ulinzi ya iliyokuwa ikiongozwa na Lamine Moro, lakini dakika 45 za kipindi cha kwanza zikamalizika matokeo yakibaki kuwa 1-0.

Kipindi cha pili Yanga ilirejea bila Lamine ambaye aliumia dakika moja kabla ya mapumziko, hivyo nafasi yake kuchukuliwa na Ditriam Nchimbi.

Dakika ya 53 David Molinga akampisha Mrisho Ngasa huku dakika tano baadaye Jaffary Kibaya akikosa bao la wazi baada ya kutanguliziwa mpira mrefu akiwa amebaki na Kipa wa Yanga, Ramadhani Kabwili shuti lake likatoka nje.

Kocha wa Yanga, Luc Eymael, alionyesha anataka bao zaidi baada ya kumtoa kiungo Abduliaziz Makame dakika ya 78 na kumuingiza Tariq Self.

Dakika tano baadaye, mpira wa adhabu ndogo uliopigwa pasi fupi ya haraka na Deus Kaseke ulizamishwa kimyani na Adeyun Saleh na kumwacha Kipa wa Mtibwa, Said Mohamed 'Nduda' akiwa hana la kufanya.

Zuber Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar alimtoa Kibaya dakika ya 84 na kumuingiza Henry Sindika kuimarisha eneo la kiungo, lakini mabadiliko hayo hayakuweza kubadili matokeo.

Yanga ilicheza dakika tano pungufu baada ya Kaseke kuonyeshwa kadi ya pili ya njano ikiambatana na nyekundu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’