Mashabiki walia na kiwango duni Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Jul 2020
Mashabiki walia na kiwango duni Yanga

Mashabiki wa klabu ya Yanga wameutaka uongozi wa timu hiyo kwa kushirikiana na wadhamini/wahisani GSM kuhakikisha wanafanya usajili wa maana ili kurejesha heshima ya mabingwa hao wa kihistoria

Wakizungumza baada ya mchezo dhidi ya Mwadui Fc ambao ulipigwa uwanja wa Taifa jana na kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1, baadhi ya mashabiki walionyesha hasira zao kwa kiwango duni cha Yanga na kusisitiza kuwa wamechoka kuingia uwanjani kushuhudia timu inayowapa maumivu kila siku

"Kusema ukweli hatuna timu, lakini hata benchi la ufundi naona hawajitambui. Unamtoaje Ngasa aliyekuwa akifanya vizuri na kuingiza wachezaji ambao kila mmoja anafahamu wana uwezo mdogo?," alisikika shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Rajabu

"Tunawaambia viongozi na GSM, hatuna haja ya kutaja majina ya wachezaji ambao hawastahili kucheza Yanga, wanawafahamu, muhimu ni kuhakikisha wanasajili wachezaji ambao watarudisha furaha yetu iliyopotea. Yanga sio timu ya kuwania nafasi ya pili, huwa inatokea tunamaliza nafasi ya pili pale tunapokosa ubingwa. Lakini kwa timu hii hata hiyo nafasi ya pili hatutaipata"

Shabiki mwingine akautaka uongozi wa timu hiyo umrudishe aliyekuwa kocha wao Mwinyi Zahera ambaye alitimuliwa mwanzoni mwa msimu

"Zahera anahitajika Yanga, kama viongozi wananisikia, kama inawezekana bora wamrudishe tu. Kwani wakati wake Yanga haikuwa mbovu kiasi hiki pamoja na kuwa ilikuwa na wachezaji wa kawaida sana tena kuliko hata hawa waliopo. Zahera alikuwa na uchungu na timu hakuwa tayari kuona timu inafungwa kizembe, ni bahati mbaya wakati ule timu haikuwa na fedha. Sasa tuna kocha mzungu lakini tunaridhika kuwania nafasi ya pili, " alizungumza shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Jackob Naimea

Kuelekea dirisha la usajili linalofunguliwa dani ya siku 11 zijazo, ni wazi viongozi wa Yanga wana deni kubwa la kuirudisha timu hiyo katika makali yake

Kwani kwa jinsi inavyocheza sasa, unaweza kusema hii ndio Yanga iliyopata matokeo duni zaidi katika kipindi cha miaka 20

Yanga ya msimu huu tayari imeweka rekodi ya kupata sare nyingi katika msimu mmoja (sare 14)

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’