Yanga imeandikisha sare ya 14 msimu huu baada ya kushindwa kupata ushindi mbele ya Mwadui Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa
Feisal Salum 'Fei Toto' aliitanguliza Yanga kwa bao safi kwenye dakika ya 27 akimalizia krosi ya winga Mrisho Ngasa kutoka upande wa kushoto
Hata hivyo ni Mwadui Fc iliyokuwa ikitengeneza mashambulizi ya hatari zaidi langoni kwa Yanga
Licha ya kwenda mapumziko wakiwa nyuma, wachimba Almasi hao wanaopambana na janga la kuteremka daraja walirejea kipindi cha pili wakiwa imara zaidi na kufanikiwa kusawazisha bao hilo kupitia kwa Yahya Mbegu
Yanga ilizinduka kwenye dakika 20 za mwisho hasa baada ya kuwaingiza mshambuliaji Yikpe Gnamien, Abdulazi Makame, Patrick Sibomana na Erick Kabamba
Lakini walishindwa kubadili matokeo na timu hizo kugawana pointi
Huo ulikuwa mchezo wa mwisho kwa Yanga kucheza jijini Dar es salaam msimu huu
Watakwenda mkoani Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar kisha kwenda Iringa kumaliza msimu dhidi ya Lipuli Fc
Yanga itashuka nafasi ya tatu kama Azam Fc itaweza kupata ushindi dhidi ya Lipuli Fc Jumapili