Kikosi cha Yanga leo kimekamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa
Mchezo huo ni wa mwisho kwa mashabiki wa Yanga wa jijini Dar es salaam kuishuhudia timu yao msimu huu kwani mabingwa hao wa kihistoria watakamilisha msimu wakiwa mikoani
Baada ya mchezo huo Yanga itakwenda mkoani Morogoro kuikabili Mtibwa Sugar na baadae kusafiri mkoani Iringa kuikabili Lipuli Fc katika mchezo ambao utapigwa Jumapili ya Julai 26
Kiungo Feisal Salum, Said Juma na Juma Abdul ambao walikosa mchezo uliopita kutokana na kadi tatu za njano, wamemaliza adhabu zao na huenda siku ya kesho kocha Luc Eymael atawajumuisha katika kikosi chake
ADVERTISE HERE